Home » » WALIMU MASWA WAPIGWA MARUFUKU SIASA

WALIMU MASWA WAPIGWA MARUFUKU SIASA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Imeandikwa na Shushu Joel, Maswa
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Maswa, Dk Fredrick Sagamiko
WALIMU wa sekondari na msingi wa shule zinazomilikiwa na serikali wilayani Maswa mkoani Simiyu wameonywa kujihusisha na siasa kwani kufanya hivyo ni kwenda kinyume na taratibu za utumishi wa umma.
Onyo hilo limetolewa jana na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Maswa, Dk Fredrick Sagamiko wakati akizungumza katika mkutano mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania( CWT) wa wilaya hiyo ya Maswa.
Alisema kuna wimbi kubwa la watumishi wa Serikali kushiriki masuala ya vyama vya siasa kwa kasi, huku walimu wakiwa wengi kinyume na Sheria za Utumishi wa Umma na watakaobainika kwenda kinyume hawataachwa.
Dk Sagamiko amepiga marufuku Idara ya Elimu Msingi na Idara ya Elimu Sekondari wilayani humo kumhamisha mwalimu bila ya ridhaa ya mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo.
Katibu wa CWT wilaya ya Maswa, Emanuel Samara alisema walimu wanadai madeni yao ya muda mrefu ya fedha za likizo na uhamisho na zinapolipwa wakati mwingine huwa ni pungufu. Chama hicho kimekabidhi mabati 520 ya Sh milioni 8.8 kwa walimu 26 waliostaafu, ikiwa ni kuwashukuru kwa utumishi wao uliotukuka.
CHANZO HABARI LEO

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Simiyu Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa