Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga
Mpina akizungumza na baadhi ya wananchi wa kijiji cha Mwagayi katika
kata ya Itinje Mkoani Simiyu wilayani Meatu, Jimboni Kisesa leo kuhusu
ongezeko la bei ya pamba ambapo kwa sasa inanunuliwa
kwa kiasi cha shilingi 1,200 kwa kilo.
Naibu Waziri Ofisi ya makmu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina, akiongena na Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Mwagayi kuhusu Ongezeko la bei ya pamba leo wananchi hao walimsimamisha Naibu Waziri Mpina alipokuwa katika ziara yake ya kikazi jimboni Kisesa.
Na Evelyn Mkokoi
NAIBU
Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Luhaga Mpina
amewataka wananchi wa Jimbo la Kisesa wilayani Meatu mkoani Simiyu
kutumia vizuri fedha wanazopata kwa kuuza pamba kununua chakula cha
kutosha na kukihifadhi ili kuondokana na uhaba wa chakula.
Akizungumza
Leo na wananchi wa Kijiji cha Mwagayi Kata ya Itinje Wilaya ya Meatu,
Mpina alisema uamuzi uliofanywa na Rais Dk John Pombe Magufuli kusimamia
ongezeko la bei ya pamba umelenga kuboresha maisha ya wananchi wanyonge
waliodhulumiwa kwa miaka mingi hivyo ni muhimu wakulima hao kutumia
vizuri ongezeko hilo la bei kuboresha maisha yao ikiwa ni pamoja na
kununua ziada ya chakula.
Mpina alisema Rais Magufuli amesimamia
na kuweka msimamo usioyumba katika suala la pamba ambapo kwa sasa bei ya
pamba imefikia shilingi 1200 kwa kilo tofauti na hapo awali ambapo
wakulima walikuwa wakidhulumiwa kwa kulipwa shilingi 600 kwa kilo na
kusababisha wananchi kuishi maisha duni na kushindwa kunufaika na zao
hilo.
“Rais Magufuli ameweka msimamo kwamba pamba isinunuliwe
chini ya shilingi 1000 na kwamba kampuni itakayoshindwa kununua kwa bei
hiyo izuiliwe kununua pamba na kufutiwa usajili wa kutonunua tena zao
hilo sehemu yoyote nchini”alisema Mpina.
Pia Mpina ambaye pia ni
Mbunge wa Jimbo la Kisesa (CCM) aliwataka wananchi hao kutumia
mabadiliko hayo ya bei ya pamba kama fursa ya kuboresha maisha badala ya
kutumia vibaya fedha hizo kwa mambo ya anasa ikiwemo kuongeza idadi ya
wake.
Alisema Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais
Magufuli imedhamiria kwa dhati kuboresha maisha ya wananchi wanyonge na
ndio sababu ya kuwekwa msimamo huo kuhusu bei ya pamba kwani kwa miaka
kumekuwa hakuna msimamo wa Serikali kuhusu zao hilo na hivyo kusababisha
wanunuzi wa pamba kujipangia bei wenyewe na kuwakandamiza wakulima.
Kuhusu
maendeleo ya jimbo hilo, Mpina alisema juhudi zinaendelea kufanyika
ikiwa ni pamoja na kumaliza kero ya maji ambapo kila kata ya jimbo hilo
itapata visima vinne vya maji ambavyo vitamaliza kero kubwa ya maji
kutokana na maeneo mengi ya jimbo hilo kuwa na ukame hasa nyakati za
msimu wa kuangazi.
Aidha Mpiana alisema kauli mbiu yake ya
‘Sitapumzika hadi maendeleo ya kweli yapatikane jimbo la Kisesa’
haijabadilika na kuwahakikishia kuwa hajawahi kuchoka,kuogopa wala
kushindwa kazi yoyote na kuwasihi kuendelea kuiunga mkono Serikali ya
awamu ya tano ili iendelee kuleta mabadiliko ambayo wananchi wameanza
kuonja matunda ya utawala wa Rais Magufuli.
0 comments:
Post a Comment