Home » » DKT MWAFFISI : MFUKO WA MAFUNZO KWA WANAHABARI NI NEEMA KWA WANAHABARI.

DKT MWAFFISI : MFUKO WA MAFUNZO KWA WANAHABARI NI NEEMA KWA WANAHABARI.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 



Na Jovina Bujulu
MAELEZO
Dar es Salaam

IMEELEZWA kuwa kuanzishwa kwa mfuko wa mafunzo  wa habari  uliopo katika muswada wa sheria ya huduma za habari utasaidia kuibua weledi, stadi, ujuzi, na ubobeaji kwa waandishi wa habari katika utelekezaji majukumu yao ya kila siku.

Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino, Dkt. Samwilu Mwaffisi wakati alipokuwa akizungumzia kuhusu maudhui yaliyopo katika muswada wa huduma za habari.

“Naunga mkono uanzishwaji wa mfuko wa mafunzo ya wanahabari kwa asilimia 100 isipokuwa mafunzo hayo yajikite katika mafunzo ya vitendo zaidi kuliko nadharia, kwani vyuo vingi tulivyonavyo nchini vinafundisha zaidi nadharia” alisema Dkt. Mwaffisi.

Akifafanua zaidi alisema kanuni zitapotungwa katika uendeshaji wa mfuko huo mkazo wake uelekezwe katika mafunzo zaidi, ambapo wanahabari wanaosomea shahada mafunzoyao  yaanze mwaka wa kwanza wa masomo yao na baada ya kuhitimu shahada ianzishwe sheria ya kusoma kwa vitendo kwa kipindi fulani.

Aidha Dkt. Mwaffisi alisema kuwa ni vyema mfuko wa mafunzo ukawajengea uwezo wanahabari katika ubobezi wa fani tofauti tofauti na hivyo kuwapa uzoefu wa kuandika fani kwa weledi zaidi.

Akizungumzia kuhusu Bodi ya ithibati inayothibitisha wanahabari, Dkt. Mwaffisi alisema jambo hilo limekuja wakati mwafaka kwani itamfanya mwandishi awajibike kwa jamii.

“Uthibitishwaji wa wanahabari utawafanya waandike kwa weledi na ufanisi zaidi wakizingatia maadili ya taaluma na jamii ili kuepuka adhabu ambayo wanaweza kupewa na bodi ya ithibati iwapo watavunja maadili” aliongeza Dkt. Mwaffisi.

MWISHO

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Simiyu Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa