KAMATI YA OLIMPIKI TANZANIA YATOA MAFUNZO YA UTAWALA NA UONGOZI WA MICHEZO SIMIYU

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

  Mkuu wa Wilaya ya Itilima, Mhe.Benson Kilangi(katikati) akizungumza na washiriki wa Mafunzo ya Utawala na Uongozi wa Michezo yaliyoandaliwa na Kamati ya Olimpiki Tanzania(TOC) wakati alipofungua mafunzo hayo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,Mhe.Anthony Mtaka Mjini Bariadi.
  Mkurugenzi Mkuu wa Mafunzo ya Utawala na Uongozi wa Michezo kutoka Kamati ya Olimpiki Tanzania(TOC) Ndg.Suleiman Jabir akizungumza na washiriki wa mafunzo hayo kutoka mkoani Simiyu (hawapo pichani) ambayo yanafanyikwa kwa muda wa siku tano Mjini Bariadi.
 Afisa Michezo wa Mkoa wa Simiyu,Ndg.Addo Komba (kushoto) akizungumza katika mafunzo ya Utawala na Uongozi wa Michezo kwa maafisa michezo, viongozi wa vyama vya michezo na walimu wa michezo yaliyoandaliwa na Kamati ya Olimpiki Tanzania(TOC).
 Baadhi ya washiriki wa Mafunzo ya Utawala na Uongozi wa Michezo yaliyoandaliwa na Kamati ya Olimpiki Tanzania(TOC) wakifuatilia Hotuba ya Mgeni Rasmi, Mkuu wa Wilaya ya Itilima, Mhe.Benson Kilangi(hayupo pichani) wakati akifungua mafunzo hayo kwaniaba ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,Mhe.Anthony Mtaka mjini Bariadi.


Na Stella Kalinga

Kamati ya Olimpiki Tanzania(TOC) imeanza kutoa mafunzo ya siku tano ya Utawala na Uongozi wa Michezo Mkoani Simiyu, ambayo yamelenga kuleta tija katika kusimamia na kuendeleza Michezo.

Mafunzo hayo yanawahusisha Maafisa Michezo Mkoa na Wilaya, Viongozi wa Vyama mbalimbali vya Michezo  na walimu wa michezo kutoka katika baadhi ya shule za msingi na sekondari mkoani Simiyu.

Mkurugenzi Mkuu wa Mafunzo hayo Ndg.Suleiman Jabir amesema lengo kuu la mafunzo hayo ni kuwasaidia Maafisa Michezo, viongozi wa vyama vya michezo ngazi ya mkoa na wilaya sambamba na walimu wa michezo kupata mafunzo ya kiufundi katika kusimamia na kuendeleza michezo, ambayo hutolewa katika mikoa yote hapa nchini, chini ya usimamizi wa Kamati ya Olimpiki Tanzania(TOC).

Akizungumzia ushiriki wa wanawake Ndg. Jabir amesema Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) imehakikisha kuwa wanawake wanashiriki kwa asilimia 40 katika mafunzo hayo ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Kamati ya Olimpiki ya Kimataifa la mwaka 2016 la kuwashirikisha wanawake katika masuala muhimu ya kimichezo ikiwemo suala la uongozi.

KATIBU MKUU NKINGA AWATAKA WADAU KUTOA MAONI YA UBORESHAJI WA SERA YA MAENDELEO YA WANAWAKE NA JINSIA TANZANIA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

 Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi Sihaba Nkinga (katikati) akifungua kikao kazi cha wadau (hawapo pichani) waliokuta kutathmini Sera ya Maendeleo ya Wanawake na Jinsia kilichofanyika katika ukumbi wa jengo la Wizara Magogoni Jijini Dar es salaam leo 9 Agosti, 2017 kulia  ni Mkurugenzi wa Mashirika yasiyokuwa ya Kiserikali Bw. Marcel Katemba (kulia) na kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Jinsia Bw. Julius Mbilinyi.
  Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Jinsia Bw. Julius Mbilinyi (aliyesimama) akibainisha malengo ya kikao cha wadau (hawapo pichani) wanaokutana kutathmini Sera ya Maendeleo ya Wanawake na Jinsia katika ukumbi wa Ofisi ndogo za Wizara ulioko Magogoni Jijini Dar es salaam leo 9 Agosti, 2017 Kulia ni Katibu Mkuu Sihaba Nkinga.
Baadhi ya wadau wanaoshiriki kikao kazi cha kutathmini Sera ya Maendeleo ya Wanawake na Jinsia kutoka taasisi mbalimbali wakifuatilia mada mbaimbali katika kikao kinachofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Wizara ulioko Magogoni Jijini Dar es salaam leo 9 Agosti, 2017.
Picha na Erasto Ching’oro WAMJW.


Na Erasto Ching’oro- WAMJW.

Katika kuhakikisha Taifa linakuwa na Sera ya Maendeleo ya Wanawake na Jinsia ambayo ni shirikishi, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imeandaa kikao kazi kwa ajili ya kukusanya maoni zaidi yatakayosaidia kuhuisha sera hiyo.

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bibi Sihaba Nkinga mara baada ya kikao na wadau kutoka taasisi mbalimbali katika mwendelezo wa mchakato wa ukusanyaji wa maoni ya ambayo yatasaidia kubaini mapungufu, na changamoto zilizopo katika Sera iliyopo na hivyo kusaidia uboreshaji wa Sera hiyo kwa kuzingatia mahitaji ya kijinsia kwa ajili ya maendeleo ya wanawake, wanaume, wavulana wasichana na watoto.

“Sera iliyopo ya Maendeleo ya Wanawake na Jinsia ya mwaka 2000 imechukua muda mrefu kufanyiwa tahmini kutokana na ukweli kuwa zoezi la tathmini linahitaji muda wa kutosha sanjari na uhakikika wa upatikanaji wa rasimali fedha kufanikisha kazi hii” alisema Bibi Sihaba.

Kwa upande wake Msauri Mwelekezi Profesa Linda Muhando aliipongeza Wizara kwa kuridhia mchakato wa kutathmini sera hiyo na kujumuisha wadau hatua amabyo itasaidia kupata mchango wa wananchi wengi zaidi na kuwezesha kupata masuala mapya amabyo hayako kwenye sera hiyo na kuyajumuisha katika rasimu ya sera inayofanyiwa mapitio.

Kikao kazi cha tathmini ya Sera hiyo kinatoa fursa kwa wadau kuibua changamoto, mapungufu yaliyopo na kuimarisha uzingatiaji wa mahitaji ya wanawake na wanaume ili kutoa fursa sawa ya upatikani haki na usawa kwa watu wote.

Maandalizi ya uboreshaji wa Sera hii utajumuisha usambazaji wa sera kwa wananchi, kutoa elimu kwa umma ili kufahamu mwongozo wa kisera, na kuiweka katika lugha nyepesi ili kujenga ufahamu wa wananchi katika wigo mpana zaidi. Aidha, ukusanyaji wa maoni ya wadau utasaidia kupanua ushirikishaji wa wananchi katika kuandaa sera na kufanikisha utekelezaji wake kwa kuzingatia wakati.

NAIBU SPIKA AFUNGUA MASHIDANO YA MBIO ZA BAISKELI MKOANI SIMIYU

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Tulia Ackson (wa pili kushoto) akimkabidhi ufunguo wa pikipiki mshindi wa kwanza kilometa 200 (wanaume), Hamisi Hussein kutoka Arusha katika mashindano ya Baiskeli yaliyofanyika Mjini Bariadi (kulia) ni Mkurugenzi Kampuni ya Jambo Food Products ambayo ni mdhamini, Mhe.Salum Khamis akimpongeza Mshindi huyo

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Tulia Ackson (mwenye bendera nyeupe kulia) akifungua mashindano ya Mbio za Baiskeli Mkoa wa Simiyu(Simiyu Jambo Festival) kwa kuruhusu washiri kuanza mashindano hayo Mjini Bariadi.

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Tulia Ackson (mwenye baiskeli wa pili kulia) akiwa na viongozi wa Mkoa na baadhi ya Wabunge wa Mkoa wa Simiyu na Viti Maalum kutoka nje ya Mkoa kwa ajili ya kufungua mashindano ya baiskeli yaliyofanyika Mjini Bariadi.
Rais wa Chama cha Baiskeli Taifa, Godfrey Mhagama akimkabidhi mshindi wa kwanza katika mbio za kilometa 10 (walemavu) katika mashindano ya Baiskeli na ngoma za asili (Simiyu Jambo Festival) yaliyofanyika Mjini Bariadi Simiyu.

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Tulia Ackson akimkabidhi ufunguo wa pikipiki mshindi wa kwanza (wanaume) katika mashindano ya Baiskeli yaliyofanyika Mjini Bariadi kilometa 200, Hamisi Hussein kutoka Arusha

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Tulia Ackson akiwa katika picha ya pamoja na washindi watatu wa mbio za Kilometa 10 (walemavu) na viongozi wa Mkoa wa Simiyu na baadhi kutoka nje ya mkoa wa Simiyu, mara baada ya kumalizika kwa mashindano ya baiskeli na Ngoma za Asili(Simiyu Jambo Festival) Mjini Bariadi.

Mshindi wa tatu mbio za baiskeli kilometa 80(wanawake), Vumilia Mwinakila kutoka Mkoa wa Simiyu akicheza wimbo wa Kisukuma pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Tulia Ackson baada ya kupokea kitita cha shilingi laki tatu.

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Tulia Ackson akiwa katika picha ya pamoja na washindi watatu wa mbio za Kilometa 80(wanawake) na viongozi wa Mkoa wa Simiyu na baadhi kutoka nje ya mkoa wa Simiyu, mara baada ya kumalizika kwa mashindano ya baiskeli na Ngoma za Asili(Simiyu Jambo Festival) Mjini Bariadi.

Washiriki wa mashindano ya mbio za Baiskeli kilometa 200(wanaume) wakiendelea kuchuana vikali kushindania pikipiki na fedha taslimu

mshindi wa kwanza kilometa 200 (wanaume), Hamisi Hussein kutoka Arusha akipanda kwenye pikipiki yake aliyokabidhiwa baada ya kuibuka mshindi dhidi ya wenzake katika mashindano ya Baiskeli yaliyofanyika Mjini Bariadi Mkoani Simiyu.

Wa pili kutoka kushoto Katibu Tawala mkoa wa Simiyu, Jumanne Sagini, Mbunge wa Busega, Mhe.Raphael Chegeni , Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Tulia Ackson wakiwa wamembeba nyoka wa kikundi cha wasanii wa ngoma ya asili ya Kisukuma.

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Tulia Ackson akimpongeza Bibi.Tatu Malulu kutoka Mwanza kwa kuwa mshindi wa pili mbio za kilometa 80 (wanawake) katika mashindano ya Baiskeli yaliyofanyika Mkoani Simiyu.

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Tulia Ackson akizungumza na waandishi wa habari katika mahojiano maalum mara baada ya kuwapokea washiriki wa mashindano ya mbio za baiskeli wa makundi yote(wanaume, wanawake na walemavu) yaliyofanyika Bariadi Mkoani Simiyu.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthny Mtaka akizungumza na waandishi wa habari katika mahojiano maalum mara baada ya kuwapokea washiriki wa mashindano ya mbio za baiskeli wa makundi yote(wanaume, wanawake na walemavu) yaliyofanyika Bariadi Mkoani Simiyu.

Mshindi wa kwanza mbio za baiskeli kilometa 200 (wanaume), Hamisi Hussein kutoka Arusha(mwenye pikipiki) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi na washindi wenzake, mshindi wa pili Masunga Duba kutoa Simiyu(wa tatu kushoto mstari wa pili) na wa tatu Richard Laizer (wa pili kulia mstari wa pili).

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Tulia Ackson(wa nne kulia) na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka(wa tatu kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na mamanju wa vikundi viwili vya ngoma za asili kimoja kinachochocheza na fisi na kingine kinacheza na Nyoka mara baada ya mashindano ya baiskeli na ngoma za asili kumalizika Mjini Bariadi.

Kikundi cha ngoma ya asili cha Wagalu kikitoa burudani kwa wananchi na viongozi waliofika kushuhudia mashindano ya baiskeli na ngoma za asili (Simiyu Jambo Festival) Mjini Bariadi Mkoani Simiyu.

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Tulia Ackson akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali pamoja na mamanju wa vikundi vya Wagika na Wagalu Mkoani Simiyu, mara baada ya mashindano ya baiskeli na ngoma za asili kumalizika Mjini Bariadi.

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Tulia Ackson(kulia) na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Kushoto wakiteta jambo wakati wakiwasubiri washiriki wa mashindano ya mbio za baiskeli yaliyofanyika Mjini Bariadi, kufika katika kituo cha mwisho.


Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Tulia Ackson(wa tatu kushoto) akicheza pamoja na baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Simiyu na waimbaji kutoka Kata ya Bumela Wilayani Itilima wakati wa kuhitimisha mashindano ya baiskeli na ngoma za asili (Simiyu Jambo Festival) Mjini Bariadi.

Baadhi ya wasanii wa Kikundi cha ngoma ya asili cha Wagika wakitoa burudani kwa wananchi na viongozi waliofika kushuhudia mashindano ya baiskeli na ngoma za asili (Simiyu Jambo Festival) Mjini Bariadi Mkoani Simiyu.

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Tulia Ackson(wa nne kulia) akicheza pamoja na baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Simiyu na Msanii Elizabeth Maliganya(wa tatu kulia) kutoka Bariadi wakati wa kuhitimisha mashindano ya baiskeli na ngoma za asili (Simiyu Jambo Festival) Mjini Bariadi.

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Tulia Ackson akiwahutubia wananchi wa Mkoa wa Simiyu mara baada ya kuhitimishwa kwa mashindano ya mbio za baiskeli na ngoma za asili (Simiyu Jambo Festival) Mjini Bariadi.

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Tulia Ackson akisalimia na Katibu Tawala Wilaya ya Bariadi, Albert Rutaihwa ara baada ya kuwasilis kwa ajili ya kufungua mashindano ya baiskeli yaliyofanyika Mjini Bariadi mkoani Simiyu.

…………………………

Na Stella Kalinga, Simiyu

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson amefungua Mashindano ya Mbio za Baiskeli na Ngoma za Asili Mjini Bariadi(Simiyu Jambo Festival) ambayo yamehudhuriwa na Maelfu ya Wananchi wa Mkoa wa Simiyu.


Mashindano hayo ya mbio za baiskeli yamehusisha kilometa 200 wanaume, kilomita 80 wanawake ambapo pia walemavu waliweza kushindania katika umbali wa kilomita tano.

Akizungumza baada ya kufungua mashindano hayo Dkt.Tulia pamoja na kuupongeza Mkoa wa Simiyu kuandaa mashindano hayo amesema, ipo michezo nchini haijapewa kipaumbele lakini ikitumiwa vizuri inaweza kutoa ajira ukiwemo mchezo wa mbio za baiskeli; ambapo ametoa wito kwa viongozi wa mikoa mingine pia kuwekeza katika michezo mbalimbali ili kuwasaidia wananchi kupata kipato.

“Lililofanyika Simiyu ni jambo jema sasa watu watakuwa wanajua kuwa wakijifua vizuri kwenye baiskeli na ngoma za jadi wanakuja kushiriki mashindano ya Baiskeli Simiyu, nitoe wito kwa viongozi wengine kufikiria mambo mengine yanayoweza kuwasaidia wananchi katika maeneo yao kupata ajira na kujipatia kipato” alisema.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka amesema mkakati wa mkoa huo ni kurasimisha tamaduni zote za Mkoa wa Simiyu na kuhusianisha na shughuli za Utalii ndani ya mkoa huo.

“Position(Nafasi) ya Mkoa wa Simiyu kwenye nchi ni kukuza tamaduni na sanaa zetu kama moja ya eneo litakalotuunganisha na sekta ya Utalii, tumezungukwa na mapori ya akiba na mbuga za wanyama, tungehitaji watalii wanapokuja kwenye maeneo hayo wapate ladha ya tofauti kiwemo utamaduni wa Mtanzania”

Mtaka ameongeza kuwa wasanii wote watatambuliwa na baadae kujengewa uwezo kupitia watalaam wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(Kitivo cha sanaa),Chuo cha Sanaa Bagamoyo na vyuo vya michezo ili waweze kufanya kazi zao kibiashara na kuimarisha uchumi wao.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kampuni ya Jambo Food Products,Mhe.Salum Khamis ambaye ndio Mdhamini wa mashindano ya Baiskeli na ngoma za Asili (Simiyu Jambo Festival) amesema ataendelea kudhamini mashindano kama hayo Mkoani Simiyu ili kuwaweseha wananchi kuinua kipato kupitia vipaji vyao.

Naye mshindi wa kwanza mbio za kilometa 80 (wanawake) Raulensia Luzuba kutoka Mwanza ameomba mashirika na makampuni mbalimbali kuwadhamini ili waweze kujengewa uwezo na kuandaliwa kushiriki katika mashindano ya Kimataifa.

Masunga Duba mshindi wa mbio za kilometa 200(wanaume)kutoka Simiyu amesema pamoja na wafadhili kudhamini mashindano ameomba pia wawasaidie wachezaji kupata baiskeli za kisasa zitakazowasaidia kwenda kwa kasi inayotakiwa.

Mashindano ya baiskeli Mkoani Simiyu yameshirikisha wachezaji kutoka mikoa ya Simiyu, Mwanza, Shinyanga,Arusha na Mbeya ambapo ushindi kwa upande wa wanaume umechukuliwa na Hamisi Hussein(Arusha) ambaye amejishindia pikipiki, wa pili ni Masunga Duba(Simiyu) kitita cha shilingi 1,000,000/= wa tatu Richard Laizer .shilingi 500,000/= na zawadi nyingine zimetolewa kwa mshindi wa nne mpaka wa 15.

Kwa upande wa wanawake mshindi wa kwanza Raulensia Luzuba kutoka Mwanza amejipatia shilingi 500,000/=, mshindi wa pili Tatu Malulu(Mwanza) shilingi 400,000/= na wa tatu ni Vumilia Mwinamila(Simiyu) shilingi 300,000/= na zawadi nyingine zimetolewa kwa mshindi wa nne mpaka wa 10.

Walemavu mshindi wa kwanza Emmanuel Mtemi amejipatia shilingi 200,000/= wa pili Masunga Sendama shilingi 150,000/= na wa tatu Saguda Sospeter shilingi 100,000/=wote kutoka mkoa wa Simiyu na zawadi nyingine zimetolewa kwa mshindi wa nne na wa tano.

WAZIRI OFISI YA MAKAMU WA RAIS AKAGUA UTEKELEZAJI WA MRADI WA CHANZO CHA MAJI CHA IGOMBE

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

 Jengo linaloonekana katika Picha ni sehemu ya kupokelea maji yanayotoka chini ya mchanga na kupanda bila pump katika mabomba ndani ya jengo hilo na kuja kusambazwa kwa wakazi kwa vijiji jirani kwa matumizi ya nyumbani
 Chanzo cha maji cha ajabu kikiwa chini ya Mchanga, ambapo juu hakuna maji yoyote yanayoonekana badala yake ni mchanga unaonekana kama mto uliyokauka maji,   chanzo hiki kipokatika kijiji cha Igombe wilayani Meatu.
 Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mungano na Mazingira Mhe.Luhaga Mpina ambaye pia ni Mbunge wa Kisesa akiongea na wadau hawapo katika picha kuhusu utekelezaji wa mradi wa chanzo cha maji cha Igombe, Mwandoya Mkoani Simiyu.
 Jengo ya la wodi ya wazazi linaloendela kujengwa katika zahanati ya Mwandoya iliyopojimboni Kisesa katika Wilaya ya Meatu.

MBUNGE WA KISESA AKUTANA NA WAKULIMA WA ZAO LA PAMBA JIMBONI KWAKE

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

 katika Picha Roli lililobeba pamba za wakulima tayari kwenda kuuzwa
 Naibu Waziri Mpina akingalia ubora wa Pamba ya wakulima katika kijiji cha Mwabusalu leo
 Naibu Waziri Mpina akipima furushi la Pamba katika Mzani Maalum kabla ya kuongea na baadhi ya wakulima wa Pamba katika kijiji cha Mwabusalu jimboni kisesa leo.
 Baadhi ya wakulima wa Pamba wakimsikiliza Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira (hayupo pichani) alipokuwa akingumzanao katika kijiji cha Mwabusalu mapema leo.
 Picha ya pamoja ya Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira ambaye pia ni Mbunge wa Kisesa na baadhi ya wakulima wa zao la Pamba kijijini Mwabusalu, Meatu Mkoani Simiyu leo.

WAUZA DAWA FEKI ZA KUUWA WADUDU WA ZAO LA PAMBA KUKIONA –MPINA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

katika Picha Roli lililobeba pamba za wakulima tayari kwenda kuuzwa
Naibu Waziri Mpina akingalia ubora wa Pamba ya wakulima katika kijiji cha Mwabusalu .
Naibu Waziri Mpina akipima furushi la Pamba katika Mzani Maalum kabla ya kuongea na baadhi ya wakulima wa Pamba katika kijiji cha Mwabusalu jimboni kisesa
Baadhi ya wakulima wa Pamba wakimsikiliza Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira (hayupo pichani) alipokuwa akingumzanao katika kijiji cha Mwabusalu mapema.
Picha ya pamoja ya Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira ambaye pia ni Mbunge wa Kisesa na baadhi ya wakulima wa zao la Pamba kijijini Mwabusalu, Meatu Mkoani Simiyu.


NA EVELYN MKOKOI – MWABUSALU MEATU

Hatua kali zitachuliwa kwa wafanyabiashara wanaouza dawa feki za kuuwa wadudu wa zao la Pamba nchini, Hayo yamesemwa leo na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina alipokuwa akizungmza na baadhi ya wakulima wa zao la Pamba katika kata ya Mwabusalu Wilayani Meatu Mkoani Simiyu, wakati wa ziara yake jimboni Kisesa.

Mpina alisema kuwa wapo wafayabiashara wanaodhoofisha wakulima wa zao la Pamba kwa kuwauzia madawa yasiyo na nguvu na kutoweza kufanya kazi kabisa katika zao la Pamba na kupelekea kufa kwa zao hilo na kuwataka watu hao kuwaletea wakulima dawa bora kabisa na kinyume na hapo wizara husika itachukua hatua dhidi yao.

Aidha amewataka wakulima wa kijiji hicho kinacholima zao hilo la mfano nakutoa mbegu Bora Pekee ya pamba nchini kuacha kilimo cha mazoea na kutumia fursa hiyo kuangalia kwanza maeneo wanayoishi kutokana na faida itokanayo na biashara ya zao la pamba kuninunulia chakula cha kutosha na kutoka kwenye nyumba za tembe na kujenga nyumba za kisasa.

Sambamba na hilo Mpina amewataka wakulima hao kuzingatia sauala la utunzaji wa mazingira kwa kuyaandaa mashamba yao kwa wakati huku wakizingatia changamoto ya mabadiliko ya tabianchi wanayokabilina nayo.

Awali, Naibu Waziri Mpina alikitembelea kiwanda cha Pamba cha Geki Investiment limited na kuutaka uongozi wa kiwanda hicho kuanza uzalishaji mapema mwakani ili wakulima wa kata ya Mwabusalu waweze kunufaika kutokanana mauzo ya pamba yao karibu. “Serikali hii inalenga katika kuinua na kuimarisha uchumi wa viwanda hivyo kiwanda hiki sasa wakati umefika wakuanza uzalishaji kisikae hapa na kutumika kama ghala kianze kazi mara moja, vinginevyo hatuta mvumilia muwekezaji huyu kama atashindwa Wizara husika itafanya kazi yake”. Alisisitiza Mpina.

Serikai ya awamu ya tano toka iingie madarakani imepandisha bei ya zao la pamba kutoka bei ya awali ya shilingi 600 kwa kilo mpaka mpaka sh. 1,200 imeelezwa kuwa kata ya Mwabusalu, ni kata ambayo imepata upendeleo kwa wakulima kuuza Pamba hiyo kwa kiasi cha shilingi 1,320 kwa kilo.

Tafiti zinaonyesha kuwa kata ya Mwabusalu inalima Pamba ambayo pamoja namatumizi mengine inatoa Mbegu ambayo inapatika pia katika maeneo mawili tuu nchini yanii mwabusalu na Ingunga Mkoani Tabora.

MPINA AWATAKA WAKULIMA WA PAMBA KISESA KUHIFADHI CHAKULA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina akizungumza na baadhi ya  wananchi wa kijiji cha  Mwagayi katika kata ya Itinje Mkoani Simiyu wilayani Meatu, Jimboni Kisesa leo kuhusu ongezeko la bei ya pamba ambapo kwa sasa inanunuliwa kwa kiasi cha shilingi 1,200 kwa kilo.

Naibu Waziri Ofisi ya makmu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina, akiongena na Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Mwagayi kuhusu Ongezeko la bei ya pamba leo wananchi hao walimsimamisha Naibu Waziri Mpina alipokuwa katika ziara yake ya kikazi jimboni Kisesa.


Na Evelyn Mkokoi 

NAIBU Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Luhaga Mpina amewataka wananchi wa Jimbo la Kisesa wilayani Meatu mkoani Simiyu kutumia vizuri fedha wanazopata kwa kuuza pamba kununua chakula cha kutosha na kukihifadhi ili kuondokana na uhaba wa chakula. 

Akizungumza Leo na wananchi wa Kijiji cha Mwagayi Kata ya Itinje Wilaya ya Meatu, Mpina alisema uamuzi uliofanywa na Rais Dk John Pombe Magufuli kusimamia ongezeko la bei ya pamba umelenga kuboresha maisha ya wananchi wanyonge waliodhulumiwa kwa miaka mingi hivyo ni muhimu wakulima hao kutumia vizuri ongezeko hilo la bei kuboresha maisha yao ikiwa ni pamoja na kununua ziada ya chakula. 

Mpina alisema Rais Magufuli amesimamia na kuweka msimamo usioyumba katika suala la pamba ambapo kwa sasa bei ya pamba imefikia shilingi 1200 kwa kilo tofauti na hapo awali ambapo wakulima walikuwa wakidhulumiwa kwa kulipwa shilingi 600 kwa kilo na kusababisha wananchi kuishi maisha duni na kushindwa kunufaika na zao hilo. 

“Rais Magufuli ameweka msimamo kwamba pamba isinunuliwe chini ya shilingi 1000 na kwamba kampuni itakayoshindwa kununua kwa bei hiyo izuiliwe kununua pamba na kufutiwa usajili wa kutonunua tena zao hilo sehemu yoyote nchini”alisema Mpina. 

Pia Mpina ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kisesa (CCM) aliwataka wananchi hao kutumia mabadiliko hayo ya bei ya pamba kama fursa ya kuboresha maisha badala ya kutumia vibaya fedha hizo kwa mambo ya anasa ikiwemo kuongeza idadi ya wake. 

Alisema Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Magufuli imedhamiria kwa dhati kuboresha maisha ya wananchi wanyonge na ndio sababu ya kuwekwa msimamo huo kuhusu bei ya pamba kwani kwa miaka kumekuwa hakuna msimamo wa Serikali kuhusu zao hilo na hivyo kusababisha wanunuzi wa pamba kujipangia bei wenyewe na kuwakandamiza wakulima.

Kuhusu maendeleo ya jimbo hilo, Mpina alisema juhudi zinaendelea kufanyika ikiwa ni pamoja na kumaliza kero ya maji ambapo kila kata ya jimbo hilo itapata visima vinne vya maji ambavyo vitamaliza kero kubwa ya maji kutokana na maeneo mengi ya jimbo hilo kuwa na ukame hasa nyakati za msimu wa kuangazi. 

Aidha Mpiana alisema kauli mbiu yake ya ‘Sitapumzika hadi maendeleo ya kweli yapatikane jimbo la Kisesa’ haijabadilika na kuwahakikishia kuwa hajawahi kuchoka,kuogopa wala kushindwa kazi yoyote na kuwasihi kuendelea kuiunga mkono Serikali ya awamu ya tano ili iendelee kuleta mabadiliko ambayo wananchi wameanza kuonja matunda ya utawala wa Rais Magufuli.

UNUNUZI WA PAMBA MWENDO WA KINYONGA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 


 UNUNUZI wa pamba katika msimu wa mwaka huu Meatu mkoani Simiyu, umedorora kulinganisha na uliopita kutokana na baadhi ya kampuni zinazonunua zao hilo kudaiwa kukosa fedha ikiwamo kushindwa kukopeshwa na benki. 

Sambamba na kukosa fedha, hali hiyo inaelezwa pia inatokana na bei ya pamba katika msimu huu kuwa kubwa hatua ambayo benki zimeshindwa kuzikopesha kampuni hizo.

Msimu wa unununzi wa zao hilo uliozinduliwa rasmi kitaifa Juni 05, mwaka huu katika kijiji cha Mwabusalu wilayani Meatu kwa bei elekezi ya Sh. 1,200 kwa kilo na jumla ya kampuni 14 zilikamilisha maadalizi ya awali ya ununuzi wa zao hilo.
Akizungumza na Nipashe juzi, Mkaguzi wa Pamba katika wilaya ya Meatu, Renatus Philbert, alisema kutokana na kudorora huko, baadhi ya kampuni zimeanza kufunga vituo vya ununuzi na kusababisha kususa kwa baadhi ya vijiji wilayani humo.

Alisema pamoja na kampuni hizo 14 kukamilisha maadalizi muhimu ya ununuzi, 12 kati ya hizo ziliingia sokoni na kuanza kununua pamba lakini zikakabiliwa na ukosefu wa fedha hivyo kushindwa kuendelea na mchakato huo.

Philbert alisema kutokana na hali hiyo, baadhi ya kampuni zimekuwa zikiwakopa wakulima huku zinapodaiwa kulipa fedha zimekuwa zikishindwa huku baadhi ya maofisa wakidaiwa kutoa lugha zisizo na staha kwa wakulima.

Pamoja na kusuasua kwa ununuzi huo, alisema baadhi ya wakulima walioko kwenye kilimo cha mkataba na uzalishaji wa mbegu, hawajaathirika kwa kuwa kampuni walizoingia nazo mkataba bado zinawapelekea fedha licha ya kusitisha ununuzi kwa baadhi ya vituo vilivyo nje ya kilimo cha mkataba.

Licha ya kuwapo kwa hali ya kusuasua, alisema baadhi ya kampuni ikiwamo Kampuni ya BioRe (T) Ltd ya Meatu, imeonyesha kumudu vyema kununua pamba inayolimwa kutokana na kilimo hai katika vituo vyake vyote 16. Alisema kampuni hiyo inanunua na kulipa fedha taslimu na kusafirisha hadi kiwandani kwa kuzingatia kanuni za zao hilo.

Chanzo:Nipashe

IGP SIRRO: MAKAMANDA WA POLISI MIKOA WATABAKI KWENYE VITUO VYAO UHALIFU UKIPUNGUA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 


PICHA B(2)
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka (kulia) akisalimiana na Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Simon Sirro mara baada ya kuwasili Mjini Bariadi kwa ajili ya ziara yake ya kikazi Mkoani Simiyu.

SIMIYU JAMBO FESTIVAL 2017 KURINDIMA MWEZI AGOSTI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 


Mashindano ya Mbio za Baiskeli katika Mikoa mitano ya Kanda ya ziwa yanataraji kufanyika AGOSTI 6, 2017 katika Viwanja vya Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Mkoani Simiyu. Mashindano hayo yameandaliwa na Kampuni ya uzalishaji wa Vinywaji Baridi ya JAMBO FOOD PRODUCT kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu.


Mashindano hayo yatahusisha Umbali wa Kilomita 200 kwa Wanaume, Kilomita 80 kwa Wanawake na Kilomita 5 kwa watu wenye Ulemavu. Pia kutakuwa na Burudani Mbalimbali Kutoka kwa WAGIKA na WAGARO na Ngoma nyingine nyingi za Asili zitatolewa siku hiyo. Zawadi Mbalimbali zitatolewa kwa washiriki ikiwemo Pikipiki na fedha Taslimu zaidi ya Shilingi Milioni nane.

Fomu za Ushiriki wa SIMIYU JAMBO FESTIVAL 2017 zinapatikana katika Ofisi za Maafisa Michezo katika Halmashauri za Mikoa ya Simiyu, Shinyanga, Mwanza, Mara na Geita kwa Gharama ya Shilingi 5000 tu.

Mgeni rasmi Katika Mashindano hayo ya mbio za Baiskeli ya SIMIYU JAMBO FESTIVAL 2017 atakuwa ni Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt Tulia Ackson Tulia.

Mkoa wa Simiyu, Wilaya Moja Bidhaa Moja

HAKUNA KIINGILIO KATIKA MASHINDANO HAYO, NYOTE MNAKARIBISHWA
 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Simiyu Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa